Marekani na Uchina zatia saini mkataba wa kibiashara

Rais wa jamhuri ya raia wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Donald Trump
Image caption Rais wa jamhuri ya raia wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Donald Trump

Marekani na Uchina wameafikiana juu ya mkataba wa kibiashara ambapo Marekani itapata nafasi ya kuuza nyama nje ya nchi.

Vingine ambavyo Marekani itaweza kuuza nje ya nchi ni gesi ya kupika na kuweza kushirikiana katika sekta ya fedha.

Kuku waliopikwa kutoka Uchina watauzwa katika masoko ya Marekani nayo Marekani itasaidia benki za Uchina kuanzisha biashara nchini humo.

Waziri wa biashara nchini Marekani, Wilbur Ross, alipongeza mkataba huo.

Alisema uliafikiwa kwa muda mfupi na utaweza kuhakikisha kuwa Marekani inauza bidhaa nyingi zaidi kwa Uchina ifikiapo mwisho wa mwaka.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii