Wanajeshi waasi Ivory Coast, waomba msamaha

Wanajeshi waasi Ivory Coast Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi waasi Ivory Coast

Maelfu ya wanajeshi nchini Ivory Coast ambao waliasi mwanzoni mwa mwaka huu wamekubali kuachana na maombi yao ya malipo zaidi toka serikalini.

Msemaji wa kundi hilo Sajenti Fofana aliomba msamaha kwa Rais Alassane Outtara mjini Abuja ikiwa ni dalili za kumaliza mgomo wao.

Waasi hao, waliilazimisha serikali kuwapa malipo zaidi ya dola elfu nane kwa kila mmoja.

Mwezi huu walipaswa kulipwa malipo mengine.

Hata hivyo wanajeshi waasi wallioko katika mji wa Bouke walikosoa mpango na kusema kuwa hawakushauriwa.

Mada zinazohusiana