Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani

Hivi ndivyo ilivyokuwa katika baadhi ya kompyuta wakati wahalifu wa mtandao walipotekeleza shambulio Haki miliki ya picha WEBROOT
Image caption Hivi ndivyo ilivyokuwa katika baadhi ya kompyuta wakati wahalifu wa mtandao walipotekeleza shambulio

Sambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia utumizi wa vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani.

Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.

Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi nchini China.

Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.

BBC inaelewa kwamba takriban mashirika 40 na huduma kadhaa za matibabu ziliathirika huku operesheni na mikutano ikifutiliwa mbali.

Programu hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola 300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.

Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.

Idadi kubwa ya kampuni kubwa ikiwemo Telefonica ,kampuni ya umeme ya Iberdrola na ile ya Gesi asilia pia ziliathirika huku kukiwa na ripoti kwamba wafanyikazi katika kampuni hizo waliagizwa kuzima kompyuta zao.

Raia walipiga picha za kompyuta zilizoathirika katika mtandao wa Twitter ikiwemo mashine ya kukata tiketi za safari ya reli nchini Ujerumani pamoja na maabara ya kompyuta nchini Italy.