Michelle Obama aukosoa utawala wa Trump

Michelle Obama aukosoa utawala wa Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Michelle Obama aukosoa utawala wa Trump

Michelle Obama ametetea vikali mipango ya kuwapatia wanafunzi vyakula bora vyenye afya alivyopigania akiwa m,ke wa rais.

Katika kongamano la afya mjini Washington ,aliushutumu uongozi wa rais Trump kwa kufutilia mbali viwango vya lishe bora inayolenga kuwafanya wanafunzi kuwa wenye afya nzuri.

''Sijui kwa nini mtu anapendelea watoto kula vyakula visivyo bora'' ,alisema.

Mmoja kati ya watoto watano nchini Marekani wanaugua ugonjwa wa kunenepa kupita kiasi, kulingana na takwimu za serikali.

Akikosoa sera za utawala wa rais Trump, bi Obama aliwaambia waliohudhuria kongamano hilo: Hapa ndipo unafaa kuangazia kuhusu malengo ya mtu.

Image caption Michelle Obama amekuwa akipigania watoto kuwa na lishe bora ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupitia kiasi miongoni mwa watoto

Lazima ujiulize kwa nini hutaki watoto wetu kula vyakula vyenye lishe bora katika shule? Na ni kwa nini hilo liwe tatizo, kwa nini hilo liingiziwe siasa? Kunaendelea nini jamani?Aliongezea: Musinishirikishe mahala popote: nipende usinipende, fikiria kwa nini mtu anapendelea mtoto wako kula chakula kibaya.

Kwa nini usherehekee, Kwa nini ufurahie kitu kama hicho? Kwa sababu hii hapa siri: Iwapo mtu anafanya hivyo hawatilii maanani watoto wenu.