Waasi 12 wa Farc wabadilika na kuwa raia Colombia

Waasi wa kundi la Farc nchini Colombia
Image caption Waasi wa kundi la Farc nchini Colombia

Waasi 12 wa kundi la Farc huko Colombia wamerudishwa katika hali ya maisha ya kiraia baada ya kuwa kundi la kwanza kukamilisa zoezi la kusalimisha silaha lililofuatiliwa na Umoja wa Mataifa.

Wanaume hao wamepokea vyeti kutoka ujumbe wa Umoja wa mataifa katika seherehe zilizofanyika huko Bogota.

Maelfu ya waasi wamesalimisha silaha tangu kundi la Farc litie saini makubaliano ya amani na serikali mwaka jana na kuidhinisha mwisho mwa mzozo wa zaidi ya miongo mitano.

Bado waasi wapatao 7000 wapo katika kambi za kujisalimisha kote Colombia wakisubiri kusajiliwa ili waweze kurudi katika maisha ya kawaida ya kiraia.