WHO kukabiliana na Ebola DRC

Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini Congo, tangu kisa cha kwanza mwaka 1976 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini Congo, tangu kisa cha kwanza mwaka 1976

Shirika la Afya Duniani, WHO limeahidi kuchukua hatua za tahadhari na haraka za haraka, ili kuzima mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola kaskazini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Inasema kuwa wataalamu wake wa kiufundi, wametumwa hadi maeneo ya vijijini, kunako aminika kutokea visa 11 vya ugonjwa wa Ebola -- zikiwemo ripoti ya vifo vya watu watatu.

Wanafanya kila mbinu kubaini upana wa mlipuko wa ugonjwa huo, kuwapa tiba walioambukizwa na virusi vya ugonjwa huo, na kuwatambua walioambukizwa au watu waliokaribiana na walioambukizwa virusi hivyo.

Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini Congo, tangu kisa cha kwanza kutambuliwa cha Ebola nchini humo mnamo mwaka wa 1976.