Trump: Nitamteua mkurugenzi mpya wa FBI haraka iwezekanavyo

Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuna uwezekano kuwa atampata mkurugenzi mpya ifikapo Ijumaa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuna uwezekano kuwa atampata mkurugenzi mpya ifikapo Ijumaa

Rais wa Mareknia Donad Trump anasema kuwa atatangaza mkurugenzi mpya wa FBI kuchukua mahala pa mkurugenzi aliyefutwa James Comey wiki ijayo.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuna uwezekano kuwa atampata mkurugenzi mpya ifikapo Ijumaa kabla ya kufanya ziara yake ya kwanza ya kigeni.

Wakili Alice Fisher alikuwa mtu wa kwanza kutahiniwa na idara ya sheria.

Kaimu mkurungeiz wa FBI Andrew McCabe, jaji ya mahakama ya mjini New York Michael Garcia na Seneta wa Republican John Cornyn pia walikutana na mku wa sheria Jeff Sessions.

Watu 11 wanaripotiwa kutajwa kwa wadhifa huo ambao utahitaji kudhinishwa na bunge la Senate.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES/REUTERS/AFP
Image caption Kutoka kushoto kaimu mkurugenzi wa FBI Andrew McCabe, Seneta John Cornyn, Jaji wa New York Michael Garcia na wakili Alice Fisher

Rais Trump amekosolewa vikali kwa kumfuta bwana Comey, ambaye amekuwa akichunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Aliwaambia waandishi wa habari wanaosafiri naye kwenye ndege ya rais ya Air Force One, kuwa anataka kufanya hima kumtaja mkurugenzi mpya wa FBI.

"Nafikiri suala hili litafanyika kwa haraka kwa sababu wote wanajulikana sana, wametahiniwa katima maisha yao, Trump alisema.