Shambulizi la komputa kuathiri watu zaidi Jumatatu

Udukuzi wa komputa kuathiri watu zaidi Jumatatu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Udukuzi wa komputa kuathiri watu zaidi Jumatatu

Wataalmu wa usalama katika mitandao ya komputa, wanaonya kwamba kunaweza kutokea mashambulio mengine sehemu mbalimbali za dunia, pale watu wataporudi makazini hapo kesho.

Inakisiwa kuwa komputa zaidi ya 120 katika nchi kama 100, zilidukuliwa Ijumaa.

Lakini polisi wa Umoja wa Ulaya wanasema walioathirika ni 200,000 katika nchi 150.

Shambulio hilo limeathiri watumizi pamoja na ofisi za serikali, kampuni zinazotengeneza magari, mabenki na huduma za afya.

Shambulio hilo limezuwia komputa kufikia data, na wanadai kikombozi, ili kuacha kuikorofisha komputa.

Uchambuzi uliofanywa na BBC katika akaunti tatu za sarafu ya kidijitali, bitcoin, unaonyesha washambuliaji wamelipwa kikombozi zaidi ya mara 100, jumla ya dola karibu 30,000.