Timu ya wasichana iliyoshinda ligi ya wavulana Hispania

Timu ya AEM Lleida girls ishinda ligi ya pili ya wanaume kwa kushinda mechi 21 kat ya 22 ilizocheza.
Image caption Timu ya AEM Lleida girls ishinda ligi ya pili ya wanaume kwa kushinda mechi 21 kat ya 22 ilizocheza.

Timu ya kandanda ya wasichana nchini uhispania imeibuka washindi katika ligi ya wanaume licha ya kutokuwepo uungwaji mkono kwa wanawake wacheza kandanda nchini humo.

Timu hiyo ya AEM Lleida girls ishinda ligi ya pili ya wanaume kwa kushinda mechi 21 kat ya 22 ilizocheza.

Mechi za kandanda zinazojumuisha jinsia zote uruhusiwa nchini Uhispania hadi wachezaji watimie miaka 14, na wasichana hawa wamecheza na wanaume tangu mwaka 2014.

Hata hivyo hakuna ufadhili kwa timu yoyote ya wanawake hadi mwaka uliopita na hata klabu maarufu nchini humo ya Real Madrid haina timu ya wanawake.

"Kuwawezesha wasichana hawa, tulihisi kuwa walistahili kucheza dhidi ya wavulana kwa sababu unahitaji wapinzani walio na uwezo ili kuweza kufanikiwa," mkurugenzi wa AEM Lleida Jose Maria Salmeron alisema.

Mada zinazohusiana