Mtu mwenye tatizo la kiakili anavyokimu mahitaji ya familia yake
Huwezi kusikiliza tena

Mtu mwenye tatizo la kiakili anavyokimu mahitaji ya familia yake

Shirika la Afya duniani linaripoti kuwa mmoja kati ya watu wanne duniani watakumbana na changamoto za afya ya kiakili maishani.

Bipolar ni hali ya kuwa na furaha sana na baada ya dakika chache unabadilika na kuwa na huzuni sana.

Ni mojawapo ya magonjwa ya kiakili, nchini Kenya ambapo takriban watu zaidi ya 800,000 wanakumbwa na hali hii mmoja wao ni Robert Njenga.

Mbali na kuishi na hali hii, anatumia kipaji cheke cha ushonaji na muziki kukimu mahitaji ya familia yake.

Swali ni je, mtu mwenye upungufu wa aina hii anaishi vipi?

Mwandishi wa BBC David Wafula amemtembelea Robert nyumbani kwake na kutuandalia taarifa hii?