Mwanamke aliyejifanya kuwa mwanamume ili kufanya kazi katika mgodi Tanzania

Pili Hussein Haki miliki ya picha UN WOMEN/DEEPIKA NATH
Image caption Pili Hussein

Pili Hussein alitamani kujiimarisha kimaisha na mawe ya thamani yanayosemekana kuwa nadra mara elfu mia moja kuliko almasi, lakini kwa kuwa wanawake hawakuwa wanaruhusiwa kwenye migodi hiyo alivalia mavazi kama mwanamume na kuwadanganya wafanyikazi wenzake kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Pili alilelewa katika familia kubwa mjini Tanzania. Mtoto wa mchugaji ambaye aliyekuwa na mashamba makubwa, babake Pili alikuwa na wake sita na alikuwa miongoni mwa watoto 38.

Licha ya hayo yote alilelewa vyema kwa njia tofauti.

''Babangu alinichukulia kama mwanamume na nilikuwa nikichunga mifugo yake, lakini sikuyapenda maisha hayo kabisa'', alisema.

Hata ndoa yake haikuwa ya furaha, akiwa na umri wa miaka 31 Pili aliikimbia ndoa yake iliyokumbwa na migogoro ya kinyumbani.

Alipokuwa akitafuta ajira alijipata katika mji mdogo wa Mererani, Tanzania, uliopo chini ya mlima mkuu wa Kilimanjaro.

Eneo hilo ni maarufu sana duniani kwa kuwa na madini nadra ya rangi ya samawati ya tanzanite.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mawe ya tanzanite yaliyopatikana mwaka 1967 na mchugaji wa kimaasai

''Sikwenda shule , kwa hivyo sikuwa na mambo mechi kuchagua,'' Pili alisema.

''Wanawake wahakuruhusiwa kwenye maeneo ya migodi hiyo, nikajitosa kama mwanamume shupavu na mwenye nguvu. Nilichukua suruali ndefu na kuzikata zikawa kama kaputula ili kufanana na mwanamume. Hivyo ndivyo nilivyofanya.''

Ili kukamilisha mabadiliko yake , alibadilisha pia jina lake.

''Niliitwa Uncle Hussein {akimaanisha mjomba Hussein}, sikumwambia yoyote kuhusiana na jina langu halisi la Pili.

Hata leo ukija katika kambi hiyo utanitafuta kwa jina hilo la Uncle Hussein.''

Kwenye migodi hiyo yenye joto ,uchafu mwingi na wenye kina cha mita mia moja chini ya ardhi Pili angefanya kazi kwa saa 10-12 kwa siku , akilima na kuchunga akiwa na matumaini ya kupata mawe hayo ya thamani kwenye mishipa ya mawe hayo ya grafiti.

''Ningeenda hadi mita 600 chini ya mgodi, mara kwa mara nikiwa shupavu kuliko wanaume wengine.

Nilikuwa na nguvu nyingi na niliweza kufanya kazi kama matarajio ya wanaume wengine wangefanya.''

Pili amesema hakuna aliyemshuku alikuwa mwanamke.

''Nilijifanya kama nyani aina ya Gorilla'' alisema, Nilipigana, lugha yangu ilikuwa mbaya , nilibeba kisu kikubwa kama Maasai.

Hakuna mtu alifahamu kwamba mimi ni mwanamke kwa sababu kile nilichokuwa nikifanya nilikifanya kama mwanamume.''

Baada ya mwaka mmoja, alipata utajiri , alipopata mawe mawili makubwa ya Tanzanite. Kutokana na pesa alizozipata alimjengea babake, mama na pacha wake nyumba mpya na akajinunulia vifaa zaidi na akaanza kuajiri wachimba migodi kumfanyia kazi.

Na kujificha kwake kuliwashawishi kwamba alichukua hatua zisizo za kawaida kwa utambulisho wake kujulikana.

Mwanamke mmoja aliripoti kwamba alikuwa amebakwa na wachimba migodi Pili akiwa miongoni mwa washukiwa.

''Polisi walipokuja, wanaume waliotekeleza ubakaji huo wakasema: 'Huyu ndio mwanamume aliyetekeleza hilo'' na nilipopelekwa katika kituo cha polisi , Pili akasema alikuwa hana namna bali kutoboa siri yake.''

''Aliwauliza polisi kumleta polisi mwanamke ili amchunguze kwamba yeye hakutekeleza kitendo hicho na baadaye aliachiliwa huru. Hata baada ya hilo wachimba migodi wenzake waliona vigumu kuamini walikuwa wamedanganyika kwa siku nyingi''.

''Hawakuamini hata polisi waliposema kwamba alikuwa mwanamke," alisema, ''haikuwa rahisi kwao kukubali hadi mwaka 2001 nilipoolewa na nikaanza familia.''

Kutafuta bwana wakati kila mtu amenizoea kama mwanamume haikuwa rahisi, Pili alipata bwana na akafanikiwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachimba migodi wakiwa kazini

Swali lililokuwa akilini mwake lilikuwa,'je ni mwanamke kweli?'' anakumbuka. ''ilimchukua miaka mitano ndipo aliponikaribia.''

Pili aliikuza taaluma yake na hivi leo anamiliki kampuni yake ya migodi ambayo ameajiri wachimba migodi 70 , watatu kati yao ni wanawake, lakini wanafanya kazi ya upishi.

Pili amesema licha ya kwamba kuna wanawake wengi katika makampuni ya migodi kuliko wakati wake, hata leo ni wanawake wachache wanaofanya kazi kwenye migodi hiyo.

''Wanawake wengine huyaosha mawe hayo , wengine ni wakala na wengine ni wapishi'' , alisema, ''lakini hawaingii ndani ya migodi , si rahisi kumpata mwanamke akifanya nilichofanya wakati wangu.''

Mafanikio ya pili yamemuezesha kuwalipia karo watoto wa ndungu zake 30 na wajukuu. Licha ya hayo amesema hawezi kumrai mwanawe kufuata nyayo zake.

''Najivunia kwa kile nilichokifanya, imenifanya tajiri lakini ilikuwa vigumu kwangu'', amesema.

''Nataka kuhakikisha mtoto wangu ataenda shule apate elimu na ataweza kujiendeleza kimaisha kwa njia tofauti mbali na nilivyopitia.''

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii