Uwezo wa kombora jipya la Korea Kaskazini

Rocket just after take-off Haki miliki ya picha KCNA

Korea Kaskazini imesema kombora ambalo ilifyatua mapema Jumapili lilikuwa la masafa marefu.

Taifa hilo limesema hilo lilikuwa kombora jipya kwa jina Hwasong-12.

Jaribio hilo la kombora lilifanikiwa na mtaalamu wa masuala ya silaha na ulinzi Melissa Hanham anasema ni ishara ya hatua zilizopigwa na Pyongyang katika kujiimarisha kijeshi.

Ndilo la karibuni zaidi la masafa marefu ya Korea Kaskazini na taifa hilo linasema kombora hilo lina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.

Picha ambazo zimetolewa na taifa hilo zinaonesha ndilo kombora lilikuwa kwenye maonesho makubwa ya kijeshi siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il-sung.

Kiongozi wa sasa Kim Jong-un alikuwepo wakati wa kurushwa kwa kombora hilo jipya kwa mujibu wa picha zilizotumwa na vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini KCNA na Rodong Sinmun.

Saa chache baada ya kurushwa kwa kombora hilo, takwimu ziliwashangaza baadhi ya wachanganuzi, kiasi cha kuwafanya waanze kutilia shaka.

Huku wasiwasi ukiwa juu rasi ya Korea, maafisa wa kikosi cha Marekani katika Bahari ya Pasifiki walikimbia kutoorodhesha kombora hilo kuwa miongoni mwa makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi bara jingine. Ingekuwa hivyo, wangekiri kwamba kombora hilo lina uwezo wa kufika Marekani bara.

Hatua moja mbele

Kombora hilo la Korea Kaskazini sasa imethibitishwa kwamba lilikuwa la masafa marefu kiwango cha wastani na lina uwezo mkubwa. Taifa hilo linasema kombora hilo lina uwezo wa kubeba bomu zito (kichwa kizito cha kombora) la nyuklia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kombora hilo la Hwasong-12 lilikuwa kwenye maonesho mwezi jana

Tamko la Pyongyang linaacha mlango wazi kuhusu uwezo hasa wa kombora hilo, ikizingatiwa kwamba hakujakuwa na ushahidi kwamba taifa hilo linaweza kuunda kichwa cha kombora (bomu) kidogo sana kuweza kutoshea katika kombora la masafa marefu.

Aidha, hakuna dalili kwamba taifa hilo litazindua kichwa kama hicho cha kombora siku za hivi karibuni.

Vyombo vya habari za Korea Kaskazini vimesema kombora hilo lilirushwa kutoka eneo la bara nchini humo na kuelekea baharini mashariki mwa rasi ya Korea ambalo lilipaa umbali wa kilomita 787 (maili 489) kutoka eneo la kuzinduliwa kwake karibu na Kusong. Kwa mujibu wa KCNA, kombora hilo lilifika kilomita 2,111.1 juu angani.

Takwimu hizi zinaoana na makadirio kwenye taarifa zilizotolewa na maafisa wa Marekani na Japan waliofuatilia kombora hilo.

Ingawa si jambo lisilo la kawaida, hali kwamba kombora hilo lilipaa juu sana kwa haraka liliwawezesha wanasayansi wa Korea Kaskazini kufanyia majaribio umbali ambao kombora hilo linaweza kwenda bila kulirusha kupitia anga la mataifa jirani.

Upeo huo unaweza kuwezesha Pyongyang kupima jinsi kombora hilo linaweza kurejea kwenye anga la dunia, chini ya joto kali, presa na msukosuko. KCNA iligusia mambo hayo kwenye taarifa yake kwa umma Jumatatu.

Njia iliyofuatwa na kombora hilo inaweza kuwa sawa na umbali wa kilomita 4,500 iwapo ingerushwa kwa kufuata njia ya kawaida. Hii ina maana kwamba kombora hilo linaweza kufikia kambi za jeshi la Marekani zilizoko Guam.

Aidha, hilo litakuwa kombora la kufika mbali zaidi kuwahi kufanyiwa majribio na Korea Kaskazini, ukiondoa makombora ya kwenda anga za juu.

Silaha ya kuogofya

Picha zinaonesha kombora hilo la Hwasong-12 ni la kurushwa kwa hatua moja na linatumia mafuta ya majimaji ambalo kwa kawaida haliwezi kufanya kazi vyema kwa umbali huo ukizingatia ukubwa wake, mafuta na jinsi ya kuchoma mafuta yake.

Kuna uwezekano kwamba sehemu kubwa ya kombora hilo inafaa kuwa sehemu ya kombora kubwa la kuruka kutoka bara moja hadi nyingine, lenye uwezo wa kufikia Marekani bara.

Haki miliki ya picha STR/AFP/Getty Images
Image caption Kim Jong-un amezidisha kasi ya majaribio ya makombora

Kwa njia hii, Korea Kaskazini inaweza kupiga hatua katika kuwa an kombora la kuruka kutoka bara hadi bara jingine, bila kuvuka mpaka uliowekwa na Twump.

Majaribio hayo ya kombora yamefanyika siku chache baada ya Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in kuingia madarakani, jambo ambalo wachanganuzi wanasema ni la kuzua hofu.

Majaribio ya makombora yameongezeka chini ya Kim Jong-un ukilinganisha na wakati wa babake na babu yake.

Hilo ni jaribio la 10 kufanyika mwaka 2017, na hili la sasa linaonesha uwezo mkubwa wa kufika mbali ukilinganisha na makombora ya awali.

Haki miliki ya picha AFP

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii