Al Shabab wavamia mji wa Mandera Kenya

Wapiganaji wa Al shabaab Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hii sio mara ya kwanza Al Shabaab kutekeleza uvamizi mji wa Mandera

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab limevamia eneo la Omar Jillo lililoko mji wa Mandera unaopakana na Somalia usiku wa kuamkia leo.

Al-Shabab limemuua afisa huyo, Chifu ws eneo Dekow Adan na kuwateka maafisa wawili wa kitengo cha polisi wa akiba kabla ya kukimbia nchini Somalia.

Vyombo vya habari vya al-Shabab vimethibitisha uvamizi huo uliotekelezwa takriban saa nne za usiku.

Serikali ya Kenya imewatuma maafisa zaidi wa usalama hadi eneo hilo huku viongozi wa usalama wakifanya mkutano wa dharura kufuatia tukio hilo.

Mji huo wa Mandera umewekewa marufuku ya kutotoka nje baada ya saa kumi na mbili jioni kufuatia ongezeko la uvamizi kutoka kundi hilo.

Tukio hilo linajiri wiki moja tu baada ya watu wawili kuuwawa katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na Al shabaab.

Visa vya utovu wa usalama vimepungua eneo hilo tangu serikali ilipoweka maafisa zaidi wa uslama.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii