Sudan Kusini yabadili jina la jeshi la nchi

Mwanajeshi wa Sudan Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Sudan Kusini wamekuwa wakikabiliana na waasi waliojitenga kwa muda sasa

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ametoa amri ya kubadili jina la jeshi la taifa hilo.

Jeshi la taifa hilo changa Afrika, linalofahamika kama Sudan People's Liberation Army, limebadili jina na kuitwa Jeshi la ulinzi la Sudan Kusini.

Sudan Kusini imechukua jina la waasi wa South Sudan Defence Force walioipa Sudan Kusini uhuru kutoka Sudan manmo mwaka wa 2011.

Mabadiliko hayo ni mojawapo ya matokeo ya makubaliano ya amani.

Wakati huo huo, rais Salva Kiir, alimrejesha kazini, Meja Jenerali Dau Aturjong Nyuol kikosini aliyetoka kikosini baada ya mapigano ya 2013.

Hata hivyo, Aturjong amerudi baada ya kujitenga na kundi la SPLA-IO linaloongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais, Riek Machar.

Aidha, Rais Kiir amefanya marekebisho zaidi kikosini na kugawanya jeshi kwa vikosi vya wanahewa, wanamaji na ardhini.

Marekebisho haya yanajiri baada ya malalamiko yaliyodai SPLA lilikuwa na ukaribu na chama tawala kuliko kuonekana kuwa jeshi la nchi linalojali maslahi ya raia wote wa Sudan Kusini.

Mada zinazohusiana