Museveni aamuru mateso kukomeshwa Uganda

Amesema kuwa Uganda imekabiliana na changamoto mbaya za kiusalama kuliko tisho kutoka kwa wahalifu wanaotumia pikipiki maarufu kama boda boda. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Amesema kuwa Uganda imekabiliana na changamoto mbaya za kiusalama kuliko tisho kutoka kwa wahalifu wanaotumia pikipiki maarufu kama boda boda.

Rais wa Uganda Yoweri Mueveni amevitaka vikosi vya usalama kuwacha kuwatesa wahalifu ikiwa wamekuwa wakifanya hivyo.

Kwa njia ya barua kwa maafisa wa ngazi za juu serikalini akiwemo waziri wa masuala ya ndani, alisema kutumia mateso kunaweza kusababisha mtu asiye na makosa kukiri na hivyo sio njia bora ya kupata ushahidi ambao unaweza kutumika mahakamani.

"Hata kama washukiwa hawatakiri makosa yao, na ikiwa wachunguzi wanaweza kufanya kazi yao vyema, kwa kutumia alama za vidole, picha, DNA, mashahidi na njia zingine za kisayansi, wahalifu wanaweza kupatikana." Alisema Museveni

Amesema kuwa Uganda imekabiliana na changamoto mbaya za kiusalama kuliko tisho kutoka kwa wahalifu wanaotumia pikipiki maarufu kama boda boda.

"Hatutashindwa kukabiliana na wahalifu wanaowaua watu ambao wameketi kwa amani ndani ya magari yao au wanaotembea barabarani.

"Hawa ni wale walifu wanaodhani kuwa wanaweza kuua na kufanikiwa kutoroka. Kwa hivyo ni lazima tuwapate kwa kutumia njia halisi na wala sio kwa mateso." Museveni aliongeza.