Mauaji ya mwandishi wa habari yasababisha maandamano makubwa Mexico

Havier Valdez alikua mstari wa mbele kupambana na madawa ya kulevya
Image caption Havier Valdez alikua mstari wa mbele kupambana na madawa ya kulevya

Maandamano makubwa yanashuhudiwa kote nchini Mexico, baada ya mauaji ya mwaandishi maarufu wa habari za upekuzi, na mshindi wa tuzo mbalimbali, Havier Valdez, ambaye alitumia miaka mingi kufichua taarifa za magenge ya walanguzi wa dawa za kulevya.

Waandhishi habari katika mji mkuu - Mexico City, wamewasilisha stakabadhi kwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, wakitaka ulinzi zaidi na haki itendeke kwa waandishi watano ambao tayari wameuawa huko Mexico katika kipindi cha miezi kadhaa ya mwaka huu.

Vyombo vya habari na watetezi wa haki za binadamu nchini humo wameungana na kuwa kitu kimoja kinachopinga tukio hilo.

Image caption Valdez alipigwa risasi katika mji huu wa Culiacan

Valderz aliandika kwa upana kuhusu watumiaji wa madawa, na Rais Enrique Pena Nieto ametaja kifo chake kama kosa la kikatili.

Mara kwa mara walichapisha sura ya Valdez ambae aliuawa karibu na ofisi za gazeti na alipatikana nyumbani kwake Culiacan katika jiji la Sinaloa.

Mexico inatajwa kama nchi ya tatu hatari zaidi kwa usalama wa waandishi wa habari duniani, huku waandishi watano wakiwa wameuawa mwaka huu.