Nchi za Caribbean ni miongoni mwa zinaongoza kwa uhalifu duniani

Zaidi ya nusu ya matukio hayo huwa hayaripotiwi.
Image caption Zaidi ya nusu ya matukio hayo huwa hayaripotiwi.

Ripoti mpya imeonyesha kuwa nchi za Caribbean ni miongoni mwa sehemu zinazoongoza kwa kuwa na uhalifu mkubwa duniani.

Benki moja inayohudumia nchi za Amerika ya Kusini, imefanya utafiti na kuhoji wahanga kutoka nchi tano za Bahamas, Trinidad and Tobago, Barbados, Jamaica na Surinam.

Katika matokeo yake, imegundua kuwa karibia robo tatu ya ndugu wa waliokufa wanasema kuwa waliwapoteza jamaa zao kwa kuuawa kikatili.

Taarifa hiyo inasema kuwa bastola hutumika zaidi katika mauji hayo ikiwa ni zaidi ya kiwango cha dunia.