Marekani yawaonya washirika wa Korea Kaskazini

Nikki Harley
Image caption Nikki Harley

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Harley ameapa kuyataja mataifa yanaounga mkono Korea Kaskazini na mpango wake wa kinyuklia huku hali ya wasiwasi ikiendelea.

''Lazima uwe unaunga mkono Korea kaskazini ama unatuunga mkono'', alisema akidai kwamba baadhi ya mataifa yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Matamshi yake yanajiri kufuatia mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Baraza hilo siku ya Jumatatu kwa pamoja lilishutumu jaribio la kombora la masafa marefu lililotekelezwa na Korea Kaskazini na kuonya kuhusu vikwazo vipya.

Korea kaskazini inesema kuwa kombora hilo lililofanyiwa majaribio ni jipya na lina uwezo wa kubeba kichwa cha kinyuklia.

Lilisafiri urefu wa kilomita 700 na kwenda juu kilomita 2000 kabla ya kuanguka magharibi mwa bahari ya Japan.

Hatahivyo Korea Kusini ilishindwa kubaini habari hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa faragha wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne , bi Harley aliyaonya mataifa yanayounga mkono Korea Kaskazini kuwacha kauli hiyo la sivyo yaone cha mtema kuni.

''Iwapo wewe ni taifa linalounga mkono Korea Kaskazini tutakutaja.Tutahakikisha kila mtu anajua wewe ni nani na tutakuwekea vikwazo hata wewe '', aliwaambia maripota akiandamana na balozi wa Japan na Korea Kusini katika umoja huo.

Washington alisema, inaunga mkono mazungumzo na Pyongyang iwapo taifa hilo litasitisha majaribio ya makombora ya masafa marefu na yale ya kinyuklia.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii