Korea Kusini: K Kaskazini imepiga hatua kwa makombora

Kombora la Korea Kaskazini
Image caption Kombora la Korea Kaskazini

Waziri wa maswala ya Ulinzi nchini Korea Kusini amesema kuwa mpango wa utengenezaji wa makombora wa Korea Kaskazini unaendelea kwa kasi zaidi ya ilivyodhaniwa.

Han Min-koo pia aliliambia bunge mjini Seoul kwamba jaribio la kombora lililofanywa na Pyongyang siku ya Jumapili liligunduliwa na na kifaa cha kutibua makombora cha THAAD nchini Korea Kusini.

Ni mara ya kwanza kwa kifaa hicho kilichotengezwa na Marekani kutumika tangu kipelekwe Korea Kusini mwezi uliopita.

China imepinga kupelekwa kwa chombo hicho ikidai kuwa kinaweza kutumika kuchunguza eneo lake.

Mjini New York, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa faragha kuzungumzia kuhusu kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.