Mmiliki wa Leicester akubali kuinunua klabu Ubelgiji

Mmiliki wa Leicester Vichai Srivaddhanaprabha Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mmiliki wa Leicester Vichai Srivaddhanaprabha

Wamiliki wa Leicester City, King Power International wamekubali kuinunua klabu ya OH Leuven ya Ubegiji.

Klabu hiyo daraja la pili iliyoko mashariki mwa mji wa Brussels , iliepuka kushushwa daraja msimu huu.

Bodi ya klabu hiyo ilikuwa imejiwekea wakati flani wa kutafuta wawekezaji na King Power ''ndio waliokuwa wametuma ombi la zabuni kwa uwazi ''.

Wakurugenzi wake walisema mkataba huo utaiwezesha kifedha na katika vigezo vya mchezo.

OH Leuven walishushwa daraja kutoka ligi ya dara la kwanza ya Ubegiji mwaka 2015-16 lakini wamesema umiliki mpya ''utawapa ufadhili wa kifedha unaotosha kama njia ya kuwasaidia kurudi katika ligi ya dara la kwanza.''

Imeongeza kwamba King Power, ilioanzishwa na mwenyekiti wa Leicester Vichai Srivaddhanaprabha mwaka 1989 itafadhili upanuzi wa mfumo wa klabu ya vijana.

Ununuzi huo utakamilishwa rasmi wakati kampuni itapokamilisha mkataba huo.

Srivaddhanaprabha anakadiriwa kuwa na thamani ya £3.6bn kulingana na jarida la Forbes

Mwenyekiti huyo mwenye umri wa miaka 58 aliinunua Leicester mwaka 2010, ambapo klabu hiyo ilifanikiwa kupanda hadi katika ligi kuu ya Uingereza miaka minne baadaye na kujinyakulia taji la ligi kuu ya Uingereza 2015-16Kindly share to help someone in need of a job placement.