Bashir aalikwa kwenye mkutano ambao utahudhuriwa na Trump

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais huyo wa Sudan anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC

Rais wa Sudan Omar al-Bashir ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kivita ICC kwa mashtaka ya uhalifu ya kivita, amealikwa kwenye mkutano nchini Saudi Arabia ambao utahudhuriwa na rais wa Marekani Donald Trump, kwa mujibu wa mashirika la AFP na New York Times.

AFP inamnukuu afisa mmoja nchini Saudi Arabia ambaye hakutajwa huku nalo gazeti la New York Times likimnukuu msemaji mmoja nchini Sudan ambaye naye hakutajwa.

Haijulikani ikiwa bwana Bashir akakubali mualiko huo.

Bwana Trump anatarajiwa kuwasili nchini Saudi Arabia siku ya Jumamosi wakati anapoanza ziara yake ya kwanza ya kigeni.

Rais huyo wa Sudan anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, kufuatia uhalifu uliotokea jimbo la Dafur. Hata hivyo amekana mashtaka hayo.

Marekani si mwanachama wa mahakama ya ICC lakini imeunga mkono kazi zake.

Mada zinazohusiana