Islamic State wavamia kituo cha runinga Afghanistan

Vikosi vya usalama Afghanistan Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi vya usalama Afghanistan

Takriban watu sita na wanamgambo wote wanne wameuawa kwenye mapigano katika jengo la kituo kimoja cha runinga kilicho mji wa Jalalabad nchini Afghanistan.

Wanne kati ya watu waliouawa walikuwa wafanyakazi wa kituo cha RTA. Polisi wawili pia waliuawa.

Shambulizi hilo lilianza wakati washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walijilipua nje ya majengo ya kituoa hicho.

Wengine waliingia ndani na kupambana na vikosi vya usalama kwa muda wa saa nne.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Vikosi vya usalama Afghanistan

Kundi la Islamic State limedai kuhusika kwenye shambulizi hilo, ambalo lilitokea karibu na ngome ya IS kwenye mpaka na Pakistan.

Wanamgambo wa Taliban pia wako eneo hilo lakini wanasema kuwa si wao walihusika.

Wafanyakazi 12 akiwemo mkuu wa kituo waliondolewa lakini wengine walikwama ndani ya jengo hilo lililo karibu na makao ya gavana wa mkoa.

Image caption Shambulizi hilo lilianza wakati washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walijilipua nje ya majengo ya kituoa cha RTA

Mada zinazohusiana