Freshley Mwamburi: Stella alikuwa mtu halisi na aliolewa na Mjapani

Nwamburi na Nduku
Image caption Freshley na mke wake wa pili Dorcas Nduku wakiwa Machakos

Wakenya katika mitandao ya kijamii leo wamechangamkia sana wimbo wa Stella Wangu wa mwanamziki mashuhuri wa humu nchini Freshley Mwamburi.

Wamechangamkia wimbo huo wakikumbuka leo hii ni tarehe 17 mwezi wa tano mwaka wa 1992 mpenzi wake wa Kenya, Stella, aliposhuka kutoka kwa ndege na mchumba wake wa urefu wa futi nne Mjapani huku amebeba mtoto mkononi.

Leo ni miaka 25 tangu siku hiyo.

Freshley anasema alitaka tu kuthibitisha ni kweli Stella ameamua kuolewa na mwalimu wake huyo huko Japan alikoenda kusomea utabibu.

Wakenya wametuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, wengine wakimkashifu Stella kwa kumtumia vibaya Freshley ambaye aliuza mifugo na shamba lake ili Stella apate nauli ya kusafiri Japan.

Huwezi kusikiliza tena
Mwamburi: Siwezi kumlaumu Stella kwa kuolewa na Mjapani

Lakini sasa Freshley amesahau yote hayo, na bado anawasiliana kwa simu na Stella akiwa Tokyo, Japan lakini anasema hamna lolote hapo kimapenzi ila ni kujuliana hali tu.

Stella sasa ana watoto wawili, naye Freshley ameoa na ana watoto wanne - wavulana watatu na msichana mmoja.

Katika wimbo wake, Freshley aliimba:

"Nilikua na mchumba wangu, tulipendana kama nyama choma

Alibahatika kwenda ngambo, chuo kikuu kwenda kusoma, miaka mitatu kule Japani kusomea udakitari, Stella wangu ehhh.

Nilivyompenda Stella jamani kajitolea kwa roho moja, nikauza shamba langu, sababu yake yeye,

Nikauza gari langu, sababu yake yeye nikauza Ng'ombe na mbuzi sababu yake yeye,

Ili apate nauli ya ndege na pesa nyngine za matumizi kule Japani,

Ilikua tarehe kumi na saba mwezi wa tano, ilikuwa tarehe kumi na saba mwezi wa tano, mwaka elfu moja tisa mia tisaini na mbili, ndiyo ilokua tarehe kamili ya Stella kurudi Kenya.

Nilikwenda uwanja wa ndege kwenda kumlaki Stella, nilikua na uncle (mjomba/au rafiki) Kilinda uwanja wa ndege.,"

Anaendelea:

"Ghafla ndege ilipotua uwanajani tuliona vituko, Stella alishuka amebeba mtoto mkononi, nyuma yake mchumba wake mfupi, futii nne Mjapani,

Nilisikitika ndani ya moyo nikakosa la kufanya,

Nilitamani nilie Kikamba lakini si kijui, ilibidii nilie Kijaluo "anatimang'owajowa",

Freshley, nilitamani nilie Kihindi lakini si kijui, ilini bidii nilie Kitaita lugha ya mama na baba,

ilinibidi nilie Kitaita, "beke mwana niponyebanda, Freshley".

Image caption Mwamburi bado anavuma kimuziki

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii