Rais wa Mexico kutoa fedha zaidi kukabiliana na uhalifu

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto
Image caption Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto ameahidi kuongeza fedha kwenye idara za serikali zinazokabiliana na uhalifu na waandishi wa habari ili kuwapa nguvu za kufanya uchunguzi.

Tamko hili limekuja baada ya maandamano yaliyoandaliwa na jumuia ya waandishi wa habari kwa nchi nzima.

Baada ya kuuawa kwa mwandishi wa habari aliyeshinda tuzo ambae alifanya uchunguzi wa miaka mingi kuhusiana na biashara na mtandao wa madawa ya kulevya.

Mwandishi huyo alipigwa risasi katika jimbo la Sinola. Hata hivyo waandishi wa habari wamesema hatua hiyo haitoshi na hairidhishi.