Macron na Tusk wakubaliana kushirikiana kwa ukaribu

Rais Macron na Donald Tusk (kushoto)
Image caption Rais Macron na Donald Tusk (kushoto)

Rais mpya wa ufaransa Emmanuel Macron, amesema ataanza kufanya kazi mapema na Rais wa jumuiya ya ulaya katika kubadilisha mfumo wa wa muongozo wake.

Macron aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari huko jiji Paris.

Mazungumzo hayo yalianza kabla ya chakula cha usiku na Tusk huku Macron akifafanua umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja katika kuleta maendeleo zaidi.

Tusk amesema kwamba mamilioni ya wakazi wa ulaya wamemuona Rais Macron kama mkombozi na ni alama ya matumaini hivyo wananchi wa jumuiya hiyo wanahitaji nguvu yake.