Trump atoa msimamo wake vikwazo dhidi ya Iran

Marekani
Image caption Rais Donald Trump wa Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani amelegeza vikwazo dhidi ya Iran kutokana na mpango wake wa nyuklia,tofauti na msimamo wa awali wakati wa kampeni.

Hatua hii ni kufuatia vikwazo dhidi ya Iran vilivyotolewa mwaka 2015 chini ya Rais Barack Obama akiungwa mkono na mataifa mengine matano yenye nguvu.

Wakati wa kampeni, Trump alitishia kufuta makubaliano hayo ambapo Iran ilikubali kupunguza kiasi chake.

Trump amesema vikwazo zaidi vinahitajika kupambana na utengenezaji wa silaha za nyuklia duniani.

Ameongeza kuwa Marekani itaweka pia vikwazo kwa maafisa pamoja na wafanya biashara kutoka China ambao wanahusishwa na mpango wa nyuklia wa Iran.