Taarifa potofu kuiponza Facebook

EU
Image caption Kamishna wa tume ya ulaya Margarethe Vestager

Tume ya Ulaya imeupiga faini mtandao wa kijamii Facebook ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni miamoja na ishirini kwa kutambua kwamba walikuwa wakiwapa maofisa wa umoja wa Ulaya taarifa potofu wakati walipokuwa wakinunua app ya ujumbe mfupi wa maneno wa WhatsApp mnamo mwaka 2014.

Tume hiyo imesema kwamba wakati wa makubaliano hayo tathimini iliyofanywa ilithibitisha kuwa hakutakuwa na muunganiko baina ya mtandao wa kijamii wa Facebook na akaunti za WhatsApp , hata hivyo mtandao huo uliendelea kuwapa wateja uchaguzi wa nini cha kufanya na hivyo kutokuwa na kizuizi.

Kamishna wa tume hiyo ya Ulaya, Margarethe Vestager, amesema kuwa hatua hiyo dalili kwamba kampuni zinapaswa kutoa taarifa sahihi.