Oxfam yawakosoa matajiri Nigeria

Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi Afrika, akiwa na bintiye Halima Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi Afrika, akiwa na bintiye Halima

Utajijri wote kwa ujumla wa watu watano matajiri zaidi nchini Nigeria wa dola bilioni 29.9 unaweza kumaliza umaskini nchini humo kwa mujibu wa shirika la Oxfam

Waziri anayehusika na masuala ya bajeti na mipango ya kitaifa nchini Nigeria Zainab Ahmed, alilishambulia shirika la Oxfam, akiikosoa ripoti yake kuhusu hali ya ukosefu wa usawa nchini Nigeria.

Mratibu wa shirika la Oxfam nchini Nigeria Celestine Okwudili Odo,alisema:

"Ni jambo lisiloeleweka kuwa mtu tajiri zaidi nchini Nigeria amejilimbikizia mali ambayo hata hawezi kuyatumia katika nchi ambapo watu milioni tano hawajui watajilisha kwa njia gani mwaka huu. Viongozi wa Nigeria ni lazima wajikakamue zaidi kukabili suala hili la umaskini."

Oxfam ilisema kwenye utafiti wake kuwa:

Mtu tajiri zaidi nchini Nigertia anapata pesa mara 8,000 zaidi kwa siku moja, kuliko pesa mtu maskini zaidi anahitaji kutumia kwa mwaka mzima.

Zaidi ya watu milioni 112 wanaishi katika hali ya umaskini nchini Nigeria, wakati mtu tajiri zaidi nchini humo na uweza wa kutumia dola milioni moja kwa siku kwa miaka 42 ili utajiri wake upate kuisha.

Licha ya ukuaji wa haraka wa uchumi, Nigeria ni moja ya nchi chache ambapo watu wanaoishi katika hali ya umaskini iliongezeka kutoka watu milioni 69 mwaka 2004 hadi watu milioni 112 mwaka 2010 ambalo ni ongezeko la asilimia 69.

Idadi ya watu matajiri nayo iliongezeka kwa asilimia 44 kwa wakati kama huo.

Oxfam iliorodhesha watu matajiri zaidi nchini Nigeria kama ifuatavyo:

  • Aliko Dangote ( Dola bilioni 14.4)
  • Mike Adenuga (Dola bilioni 9.9 )
  • Femi Otedola (Dola bilioni 1.85 )
  • Folorunsho Alakija (Dola bilioni 1.55 )
  • Abdul Samad Rabiu (Dola bilioni 1.1 ).

Mada zinazohusiana