Aliyejaribu kumbusu nyoka aumwa usoni Marekani

Nyoka huyo anaaminika kutokeka baada ya kisa hicho. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nyoka huyo anaaminika kutokeka baada ya kisa hicho.

Mwanamume mmoja katika jimbo la Florida nchini Marekani ambaye alijaribu kumbusu nyoka na badala yake nyoka huyo akamuuma, anaendelea kupata matibabu hospitalini.

Nyoka huyo alipatwa na Charles Goff, mkaazi wa kaunti ya Putnam kaskazini mwa jimbo la Florida siku ya Jumatatu.

Siku moja baadaye jirani wake ambaye alitajwa na kituo cha CBS kama Ron Reinold alianza kucheza nyuko huyo kwa kujaribu kumbusu.

Bwana Reinold alisafirishwa kwa njia ya ndege na kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini,.

Kijana mmoja alisema, "nitambusu mdomoni," ndipo nyoka huyo akamuuma usoni, bwana Goff alililiambia shirika la habari la Action News Jax.

Kituo cha First Coast News kilisema kuwa muathiriwa alikuwa na fahamu lakini katika hali mbaya. Nyoka huyo anaaminika kutokeka baada ya kisa hicho.

Haijulikani sababu iliyochangia bwana Reinold ajaribu kumbusu nyoka huyo.