Feri ya Korea Kaskazini yatia nanga Urusi

Feri hiyo inayojulikana kama Mangyongbong, itasafiri mara moja kwa wiki Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Feri hiyo inayojulikana kama Mangyongbong, itasafiri mara moja kwa wiki

Feri moja ya abiria ya korea kaskazini imetia nanga katika bandari moja iliyo mbali mashariki mwa urusi ya Vladivostok kwa mara ya kwanza.

Feri hiyo inayojulikana kama Mangyongbong, itasafiri mara moja kwa wiki kuenda bandari hiyo na pia itabeba mizigo.

Korea Kaskazini iko chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa

Huduma hizo za feri zinakuja huku kukiwa na msukosuko kati ya Korea Kaskazini na Marekani kufuatia majaribio ya silaha za nuklia za Korea Kaskazini.

Feri hiyo ina mkahawa, baa na eneo la kupigia muziki.

Image caption Watalii wa kichina wanatarajiwa kutumia huduma hiyo kuzuru taifa la Korea Kaskazini na Urusi.

Watalii wa kichina wanatarajiwa kutumia huduma hiyo kuzuru taifa la Korea Kaskazini na Urusi.

Kampuni moja ya Urusi ya InvestStroiTrest inasimamia huduma za feri hiyo kutoka badari ya Korea Kaskazini ya Rajin.

Uhusiano wa karibu wa kiuchumia kati ya Urusi na Korea Kaskazini ulianza wakati wa vita baridi, wakati wakiwa washirika kukabiliana na nchi za magharibi.

Gazeti la serikali la kila siku la Urusi la Rossiiskaya Gazeta, linasema kuwa Mangyongbong itabeba bidhaa muhimu ambavyo vitakaguliwa na maafisa wa forodha wa Urusi.