Gari lagonga na kujeruhi watu 19 New York

Gari lagonga na kuua mtu 1 na kujeruhi 19 New York Haki miliki ya picha EPA
Image caption Gari lagonga na kuua mtu 1 na kujeruhi 19 New York

Mtu mmoja ameuawa na wengine 19 kujeruhiwa wakati gari liliendeshwa kuenda sehemu ya kupitia watu eneo la Times Square mjini New York, Marekani.

Dereva wa gari hilo amekamatwa na eneo hilo kufungwa kwa mujibu wa idara ya polisi ya mji wa New York.

Gari hilo linaripotiwa kuruka vizuizi kwenye mtaa wa 45 katika eneo maarufu la watalii.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiondolewa eneo hilo.

Picha zilionyesha gari nyekundu aina ya Honda likiwa limepinduka huku likifuja moshi

Dereva wa gari hilo mwenye umri wa miaka 26 anafanyiwa uchunguzi wa pombe.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiondolewa eneo hilo.

Anaripotiwa kuwa na historia ya kuendesha gari akiwa mlevi.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiondolewa eneo hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Picha zilionyesha gari nyekundu aina ya Honda likiwa limepinduka huku likifuja moshi

Polisi wanasema kuwa dereva alipoteza mwelekeo na huenda kisa hicho kinaonekana kuwa ajali.

Waliongeza kuwa kisa hicho hakina uhusiano na ugaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wanasema kuwa dereva alipoteza mwelekeo na huenda kisa hicho kinaonekana kuwa ajali.