Michel Temer: sitojiuzulu kwa kashfa ya rushwa

Temer amekuwa marakani tokea kuondolewa madarakani kwa mtangulizi wake Dilma Rousseff kwa kashfa ya rushwa Agosti 31, 2016
Image caption Temer amekuwa marakani tokea kuondolewa madarakani kwa mtangulizi wake Dilma Rousseff kwa kashfa ya rushwa Agosti 31, 2016

Rais wa Brazil Michel Temer amesema kamwe hawezi kujiuzulu kutokana na kashfa ya malipo ya fedha nyingi kama yaliyochukuliwa kama rushwa.

Katika mahojiano mafupi kwa njia ya Televisheni, Temer hana la kuogopa kutokana na uchunguzi juu yake ulioamriwa na mahakama kuu.

Amesema hajafanya jambo lolote baya na kwamba tuhuma hizo zitarudisha nyuma juhudi zake za kuimarisha uchumi uliodorora.