Kiongozi wa upinzani Venezuela apokonywa hati ya kusafiria

Capriles pia anahudumu kama gavana wa jimbo la Miranda
Image caption Capriles pia anahudumu kama gavana wa jimbo la Miranda

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Venezuela Henrique Capriles amesema alipokonywa hati yake ya kusafiria uwanja wa ndege alipokuwa akijiandaa kwenda New York.

Alipanga kukutana na viongozi wakuu wa UN kujadili mgogoro wa kisiasa na uchumi unaoikumba nchi yake.

Capriles amekuwa muhimili wa kuchochea maandamano yanayoendelea nchini Venezuela.

Miezi miwili iliyopita alifungiwa kushiriki kwenye siasa kwa miaka 15 kwa tuhuma za kuleta uchochezi.

Katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za Amerika Luis Almagro amesema kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za binaadamu.