Watu 60 wauawa kusini mwa Libya

Wapiganaji nchini Libya Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji nchini Libya

Habari kutoka Libya, zinasema kwamba takribani watu 60 wameuawa, katika mapigano makali kati ya makundi mawili hasimu, Kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa kundi la Libyan National Army, amesema kuwa uwanja wake wa ndege wa Brak al-Shati, ulivamiwa.

Kundi moja linalojiita Third Force, linasemekana ndilo lililotekeleza shambulio hilo.

Eneo hilo limekuwa likiangaziwa pakubwa kutokana na taharuki inayotanda kati ya wanaounga mkono serikali inayotambuliwa na Umoja wa mataifa iliyoko katika mji mkuu Tripoli, na wapinzani wao.

Mapema mwezi huu, kamanda mkuu wa Libyan National Army, Khalifa Haftar, alikutana na kiongozi mkuu wa serikali iliyopo Tripoli, Bwana Fayez al-Sarraj, ili kujaribu kuzima uhasama unaotokota Kusini mwa nchi hiyo.

Image caption Ramani ya Libya

Libya iliingia vitani baada ya kuangushwa kwa utawala wa hayati Kanali Muammar Gaddaffi mnamo Oktoba 20 mwaka 2011.