Serikali ya Japan yamruhusu mfalme Akihito kujiuzulu

Mfalme Akihito wa Japan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfalme Akihito wa Japan

Serikali ya Japan, imeidhinisha mpango wa kumruhusu mfalme Akihito wa nchi hiyo, ajiuzulu.

Baraza la Mawaziri limeunga mkono mpango huo, ambao sasa utapelekwa bungeni ili uweze kuidhinishwa.

Mwaka jana mfalme huyo mwenye umri wa miaka 83, alielezea azma yake ya kuachia mamlaka kwa sababu za kiafya.

Amekuwa utawalani tangu mwaka 1989.

Iwapo hatua hiyo itaidhinishwa na kufaulu, atarithiwa na mwanawe Prince Naruhito.

Taarifa zasema kuwa atakabidhiwa mamlaka mwaka ujao wa 2018.

Mada zinazohusiana