Mwamburi: Siwezi kumlaumu Stella kwa kuolewa na Mjapani
Huwezi kusikiliza tena

Freshley Mwamburi: Siwezi kumlaumu Stella kwa kuolewa na Mjapani

Wakenya Jumatano walimiminika kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii kukumbuka siku msanii Freshly Mwamburi alivyosikitika kuona mpenzi wake Stella ametua uwanja wa ndege mjini Nairobi, mtoto mikononi na mchumba wake Mjapani.

Ilimbidi Freshley atunge wimbo wa kumbukumbu, Stella Wangu, kwani ni siku ambayo hataisahau maishani mwake.

Hata hivyo anasema haja tatizo kwamba Stella, ambaye anasema sasa ni daktari Japan, alimwacha na kuolewa na Mjapani.

Mwamburi mwenyewe ameoa wake wawili na ana watoto.

Mwandishi wa BBC John Nene amezungumza naye na kutuandalia ripoti hii.

Mada zinazohusiana