Afrika wiki hii kwa picha : 12 - 18 Mei 2017

Baadhi ya picha bora kutoka barani Afrika na zile za Waafrika wakiwa sehemu mbali mbali duniani.

Mchuuzi awauzia wapita njia na wenye magari panya waliochomwa eneo la Salima, malawi siku ya jumatatu. Panya waliochomwa wanapendwa sana na watu nchini Malawi na biashara yake imenoga sana hasa vijijini. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mchuuzi akiwauzia wapita njia na wenye magari panya waliochomwa eneo la Salima, Malawi, siku ya Jumatatu. Panya waliochomwa wanapendwa sana na watu nchini Malawi na biashara yake hunoga sana hasa vijijini.
Kobe huyo aina ya 'ploughshare' alifikishwa mbele ya wanahabari karibu na uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur huko Sepang, Malaysia. Kobe hao 330 walikuwa wamewekwa kwenye masanduku amabayo yalidhaniwa kusafirisha mawe kutoka uwanja wa ndege wa Antananarivo, nchini Madagascar. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku hiyo hiyo kobe huyu wa aina ya 'ploughshare' aliokolewa nchini Malaysia baada ya kusafirishwa kinyemela kutoka Madagascar. Maafisa walipata kobe 330. Kobe hao walikuwa wamewekwa kwenye masanduku amabayo yalidhaniwa kusafirisha mawe kutoka uwanja wa ndege wa Antananarivo, nchini Madagascar.
Picha iliyopigwa tarehe 13 Mei, 2017, inaonyesha maiti moja iliyohifadhiwa katika wilaya ya Touna el-Gabal, mkoani Minya. Waakiolojia wamezipata maiti hizo 17 zisizo za kifalme katika jangwa. Kando ya maiti hizo, kulikuwa na nakala ya dhahabu iliyochapishwa zamani sana. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku ja Jumamosi, wanahabari waliruhusiwa kupiga picha za miili ya watu waliofariki zama za kale iliyohifadhiwa huko Misri. Waakiolojia waliipata miili 17 isiyo ya watu wa familia ya kifalme katika jangwa. Kando ya maiti hizo, kulikuwa na makala ya dhahabu iliyochapishwa zamani sana.
Mwendeshaji pikipiki wa motocross afanya sarakasi katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya kuwepo kwa jimbo la Lagos, nchini Nigeria, tarehe 13 Mei, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku hiyo hiyo mwendeshaji pikipiki wa mashindano ya pikipiki wa Afrika Kusini aliwatumbuiza watu waliofika kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya kuwepo kwa jimbo la Lagos, nchini Nigeria.
Wakimbizi kutoka Sudan kusini wanajenga nyumba katika kambi ya UNHCR, eneo la al-Algaya katika jimbo la White Nile, kusini mwa Khartoum tarehe 17 Mei, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ujenzi unaendelea katika kambi ya wakimbizi wa kutoka Sudan kusini katika eneo la al-Algaya, nchini Sudan, siku ya Jumatano.
Siku ya jumatatu, mwanamke ameketi karibu na mahakama ya kikatiba mjini Johannesburg, Africa Kusini, amabako kulikuwa na maandamano ya kumtaka Rais Jacob Zuma aondoke mamlakani tarehe 15 Mei, 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Siku ya Jumatatu, mwanamke huyu alikuwa ameketi karibu na mahakama ya kikatiba mjini Johannesburg, Afrika Kusini, ambako kulikuwa na maandamano ya kumtaka Rais Jacob Zuma aondoke mamlakani.
Mkulima amshika kondoo wa aina ya Merino kwenye soko la kilimo barani Afrika huko Bothaville, tarehe 16 Mei, 2017 huko Bothaville, Afrika Kusini. Wageni elfu 70 wanatarajiwa kuhudhuria maonyesho hayo. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakulima wajitayarisha kuuza mifugo wao kwenye maonyesho katika soko kubwa zaidi la kilimo barani Afrika huko Bothaville, Afrika Kusini siku ya Jumanne.
Askari anaonekana katika makazi ya zamani ya aliyekuwa Rais wa DRC Mobutu Sese Seko tarehe 15 Mei, 2017, eneo la Nsele, kilomita 40 nje ya Kinshasa. Sese Seko alifukuzwa na vikosi vya waasi wakiongozwa na Laurent-Desire Kabila mwaka wa 1997 baada ya miaka 32 ya utawala. Alikufa miezi mitatu baadaye huko Morocco. / AFP Haki miliki ya picha AFP
Image caption Askari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anatazama michoro ya grafiti kwenye kuta za ikulu ya zamani ya rais, siku ya Jumatatu...
Askari anaonekana katika makazi ya zamani ya aliyekuwa Rais wa DRC Mobutu Sese Seko tarehe 15 Mei, 2017, eneo la Nsele, kilomita 40 nje ya Kinshasa. Sese Seko alifukuzwa na vikosi vya waasi wakiongozwa na Laurent-Desire Kabila mwaka wa 1997 baada ya miaka 32 ya utawala. Alikufa miezi mitatu baadaye, huko Morocco. / AFP / AFP PHOTO / JOHN WESSELSJOHN WESSELS/AFP/Getty Images Haki miliki ya picha JOHN WESSELS
Image caption Ikulu hiyo ya zamani iliyokuwa makao ya Rais wa zamani wa DRC Mobutu Sese Seko inapatikana Nselel, kilomita 40 nje ya mji mkuu Kinshasa.
Sese Seko alifukuzwa na vikosi vya waasi wakiongozwa na Laurent-Desire Kabila mwaka wa 1997 baada ya miaka 32 ya utawala. Alikufa miezi mitatu baadaye katika Mei 1997. / AFP Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sese Seko alifukuzwa na vikosi vya waasi wakiongozwa na Laurent-Desire Kabila mwaka wa 1997 baada ya miaka 32 ya utawala. Alikufa miezi mitatu baadaye, huko Morocco.

Picha ni kwa hisani ya AFP, EPA, Getty Images na Reuters