Trump azuru Saudia, huku joto la kisiasa likimkabili nyumbani

Trump awasili nchini Saudia ambapo anaanza ziara ya mataifa 8 ya kigeni
Image caption Trump awasili nchini Saudia ambapo anaanza ziara ya mataifa 8 ya kigeni

Mikataba ya mabilioni ya madola kati ya Marekani na Saudia itatiwa saini siku ya Jumamosi wakati ambapo rais Trump anafanya ziara yake ya kwanza ya kigeni Saudia.

Bwana Trump na mkewe Melania walipokewa na mfalme wa Saudia Salman Jumamosi alfajiri.

Swala kuu linalotarajiwa kuzungumziwa kwenye kikao hicho ni vipi kukabliana na itikadi kali zinazosababisha vitendo vya kigaidi.

Ziara hiyo ya siku nane pia itashirikisha Israel, Palestina,Ubelgiji,Vatican na Sicily.

Ziara hiyo inajiri wakati ambapo bwana Trump anakabiliwa pigamizi kali nchini mwake kufuatia hatua ya kumfua kazi mkurugenzi wa shirika la FBI James Comey.

Amekosoa vikali uamuzi wa kumteua mtaalam kuchunguza ushawishi wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Bwana Trump anaandamana na mwanawe Ivanka,mshauri wa ikulu ya Whitehouse pamoja na mumewe Jared Kushner ambaye ni mwanamacha muhimu wa baraza la mawaziri la rais Trump

Kama waziri mkuuwa wa Uingereza Theresa May na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusu ziara zao za hivi karibuni nchini Saudia, bi Trump na Ivanka hawakuvaa hijab.