Japan yaajiri asilimia 97 ya waliohitimu chuo kikuu

Japan imeripoti rekodi ya kiwango cha juu cha ajira kwa raia wake wanaohitimu elimu ya chuo kikuu hasa vijana.
Image caption Japan imeripoti rekodi ya kiwango cha juu cha ajira kwa raia wake wanaohitimu elimu ya chuo kikuu hasa vijana.

Japan imeripoti rekodi ya kiwango cha juu cha ajira kwa raia wake wanaohitimu elimu ya chuo kikuu hasa vijana.

Zaidi ya asilimia tisini na saba ya vijana ambao hufuzu katika muhula wa mwaka huu wamepata ajira.

Hicho ndio kiwango cha juu zaidi cha ajira kurekodiwa tangu mwaka wa 1997.

Awali utafiti ulionesha kulikuwa na uhaba wa wafanyikazi wanaohitajika kutokana na sera ya Japani kutopendelea wafanyikazi wa kigeni.

Hilo liliwalazimu waajiri kuwaandika kazi hata wanafunzi wa madarasa ya juu katika shule za secondari

Uchumi wa Japan umeonyesha dalili nzuri za kuboreka baada ya kudumaa miaka mingi.