Mwanamke amkata uume mwalimu wa dini aliyembaka India

Wanarakati nchini India wamekuwa wakipinga idadi kubwa ya visa vya ubakaji Haki miliki ya picha SAJJAD HUSSAIN/AFP/GETTY IMAGES
Image caption Wanarakati nchini India wamekuwa wakipinga idadi kubwa ya visa vya ubakaji

Mwanamke wa miaka 23 nchini India amezikata sehemu 'nyeti' za mwalimu wa kufunza dini katika jimbo la kusini la Keral kwa kudai kuwa alimbaka kwa miaka mingi.

Polisi wanasema kuwa mshukiwa anayejulikana kama Gangeshananda Theerthapada alikuwa akizuru katika nyumba ya mwanamke huyo ili kumfanyia matambiko ya ibada babake mwanamke huyo aliyekuwa mgonjwa.

Mamake alitumai kwamba jamaa huyo aliyejidai kuwa mtakatifu atandolea familia hiyo matatizo.

Badala yake ,mwanawe anasema alikuwa akimbaka kila anapotembea nyumba hiyo

Siku ya Ijumaa usiku, alichukua kisu na kumshambulia alipojaribu kumbaka na baadaye akaita maafisa wa polisi.

Mbakaji huyo baadaye alikimbizwa hadi katika taasisi ya elimu ya matibabu ya Thiruvananthapuram ili kufanyiwa upasuaji wa dharura

Hopsitali hiyo ilisema katika taarifa : Mtu mwenye umri wa miaka 54 alilazwa katika hospitali hiyo siku ya Jumamosi.

''Asilimia 90 ya uume wake ulikuwa umekatwa na hakuna njia ya kuushona na kuurudisha mahala pake''.

Wapasuaiji katika hospitali hiyo walimfanyia upasuaji wa dharura ili kuzuia damu iliokuwa ikimwagika na kumwezesha kupitisha mikojo.