Dadake Prince kurithi mali yake

Mwaka mmoja baada ya kifo cha mwanamuziki mashuhuri Prince, dadake na nduguze wa kambo watano , wametangazwa kama warithi wake halali.
Image caption Mwaka mmoja baada ya kifo cha mwanamuziki mashuhuri Prince, dadake na nduguze wa kambo watano , wametangazwa kama warithi wake halali.

Mwaka mmoja baada ya kifo cha mwanamuziki mashuhuri Prince, dadake na nduguze wa kambo watano , wametangazwa kama warithi wake halali.

Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama moja katika jimbo la Minnesota nchini Marekani, ambako Prince alifariki akiwa katika studio yake ya Paisley Park baada ya kunywa kimakosa dawa nyingi za kuondoa maumivu.

Prince hakuwa ameacha maagizo ya maandishi kuhusu nani mrithi wake , hivyo kukachipuka wengi waliodai kuwa na uhusiano nae wa kidugu au kirafiki waliodai wagawiwe fedha na mali zake zenye thamani ya ma millions ya dola.

Katika makabiliano ya mahakamani takriban watu 45 walijitokeza kudai mali yake ikiwemo mfungwa mmoja katika eneo la Colorado anayedai kuwa mwana wa Prince.

Mnamo mwezi JUlai mwaka uliopita, jaji mmoja alikataa madai ya watu 29 na kuagiza kufanyiwa vipimo vya jeni.

Mali ya Prince inashirikisha mali kadhaa na haki ya muziki ikiwemo vibao kama vile Let Go Crazy n When Doves Cry pamoja na nyimbo nyengine ambazo hazijatolewa.

Jaji wa wilaya Keivn Eide alisema kuwa wale walionyimwa urithi lazima wapewe muda wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.