Watu milioni 2 wajiandikisha kupiga kura Uingereza

Raia wa kike Uingereza akitoka kupiga kura kituoni
Image caption Raia wa kike Uingereza akitoka kupiga kura kituoni

Zaidi ya watu milioni 2 wamejiandikisha kupiga kura, tangu waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May alipotangaza mipango ya kupiga kura kabla ya siku ya uchaguzi mkuu kufika hapo June tarehe 8.

Idadi kubwa ya waliojiandikisha ilikuwa April 18, siku ambayo waziri huyo mkuu alipotoa tangazo hilo, ambapo zaidi ya watu 150,000 walijiandikisha.

Idadi ya vijana waliojiandikisha ni kubwa mno kuliko watu wa umri mwingine.

Siku ya mwisho ya kujiandikisha moja kwa moja mtandaoni ni Jumatatu adhuhuri, Mei 22.