Wakamatwa na madawa ya Kulevya Brazil

Ramani ya Brazil
Image caption Ramani ya Brazil

Polisi nchini Brazil wamewakamata takriban watu 40, kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika mji wa Sao Paulo, Cocaine imekuwa ikiuzwa na kununuliwa bila kificho.

Mamia ya polisi waliokuwa na silaha nzito walishiriki katika operesheni hiyo.

Zoezi hilo lilikumbwa na vurugu za waathirika wa madawa hayo, huku matukio ya wizi katika maduka na uharibifu wa magari ukitokea.

Meya wa Sao Paulo Joao Doria amesema operesheni hiyo imekamilisha zoezi la kuliokoa eneo hilo.

Hata hivyo wakosoaji wanasema hatua hiyo itasababisha tatizo hilo kuhamia maeneo mengine ya mji.