Korea Kaskazini yakiri kufanya jaribio lingine la Kombora

Picha za jaribio la kombora hilo zilichapishwa na gazeti la Korea Kaskazini Haki miliki ya picha Rodong Sinmun
Image caption Picha za jaribio la kombora hilo zilichapishwa na gazeti la Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imekiri kuwa ilifanikiwa kurusha kombora la masafa ya wastani siku ya Jumapili.

Shirika la habari la taifa nchini humo KCNA lilisema kuwa zana hiyo sasa iko tayari kutumiwa kwa shughuli za kijeshi.

Ikulu ya White House ilisema kuwa kombora hilo lilikuw la masafa marefu kuliko makombora yaliyotumiwa na Korea Kaskazini wakati majaribio matatu ya awali.

Jaribio hilo linakuja wiki moja baada ya Korea Kaskazini kufanyia jaribio kile ilichokitaja kuwa kombora mpya lenye uwezo wa kubeba silaha ya nuklia.

Jumatatu iliyopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa Korea haistahili kufanya majaribio zaidi.

Haki miliki ya picha Rodong Sinmun
Image caption Kim Jong-un alikuwa eneo jaribio hilo lilifanyika

Sasa baraza hilo linatarajiwa kukutana kwa faragha siku ya Jumanne kwenye mkutano ulioitishwa na Marekani, Korea Kusini na Japan.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alishuhudia shughuli ya jaribio la kombora la Pukguksong-2 siku ya Jumapili

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Korea Kusini imelitaja jaribio hilo kuwa la kiholela huku waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani akilitaja kuwa la kughadhabisha.

Kombora hio lilisafiri umbali wa kilomita 560 kuelekea bahari ya Japan. Kombora la wiki iliyopita lilisafri umbali wa kilomita 700.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kombora la Pukguksong-2, pia lilifanyiwa majiribio mwezi Februari