Msaada wa kimataifa wa kuachiwa kiongozi wa upinzani Zambia

Mashtaka hayo yanatokana na kile kinachotajwa kuwa hatua ya Hichilema kuzuia msafara wa magari ya Rais. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashtaka hayo yanatokana na kile kinachotajwa kuwa hatua ya Hichilema kuzuia msafara wa magari ya Rais.

Mke wa kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia kuachiliwa kwa mumewe.

Mutinta Hichilema anasema kuwa kudorora kwa demokrasia nchini mwake, na nchi hiyo kutumbukia kwenye utawala wa kiimla ni jambo ambalo haliwezi kupuuzwa.

Alitoa matamshi hayo wakati serikali ya Uingereza ilisema kuwa wawekezaji wanatiwa hofu na kuendelea kuzuiwa kwa mumewe kutokana na mashtaka ya uhaini.

Leo hii jaji anaratarajiwa kuamua ikiwa kesi hio itatupiliwa mbali au ipelekwe kwenye mahakama ya juu.

Mashtaka hayo yanatokana na kile kinachotajwa kuwa hatua ya Hichilema kuzuia msafara wa magari ya Rais.