Mwanamuziki mwenye bendi ya mtu mmoja Kenya

Mwanamuziki mwenye bendi ya mtu mmoja Kenya

Joshua Kamau, maarufu kama ‘Krackwizz’, ni mwanamuziki wa kujitegemea jijini Nairobi ambaye ameunda bendi yake mwenyewe.

Anafahamika sana kwa kutumbuiza watu mitaani Nairobi akitumia mseto wa ala zake ambazo kwa pamoja zina uzani wa kilo 10.

Anaweza kucheza zaidi ya ala 12 za muziki kwa wakati mmoja zikiwemo gitaa, ngoma na hamonika.