Waliokuwa waasi waanzisha tena vurugu Ivory Coast

Waasi hao wa zamani wanataka walipwe pesa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi hao wa zamani wanataka walipwe pesa

Mamia ya waliokuwa waasi waliingia kwenye mitaa ya mji wa Bouake nchini Ivory Coast, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa chini humo wakiitaka serikali iwalipe.

Shirika la AFP lilisema kuwa waasi hao walivuruga mazishi yaliyohudhuriwa na waziri mmoja

Wairi huyo alikuwa amejitolea kuwasaidia zaidi ya waasi 6000 wa zamani kubuni biashara.

Wanajeshi waasi Ivory Coast, waomba msamaha

Wanajeshi waasi wafyatua risasi Ivory Coast

Milio ya risasi yasikika kambi za jeshi Ivory Coast

Lakini kile walichapewa kiliwakasirisha waasi waliopiga kelele wakisema kuwa wanataka kulipwa pesa, ambapo walilizingira gari la waziri wa uzalendo na kulizuia kuondoka.