Baraza la Usalama la UN lailaani Korea Kaskazini

Makombora ya Korea Kaskazini Haki miliki ya picha RODONG SIN MOON
Image caption Makombora ya Korea Kaskazini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelani vikali jaribio la hivi karibuni la makombora lililofanywa na Korea kaskazini.

Katika taarifa iliyotolewa na baraza hilo, limeelezea jaribio hilo, kama la ''kuvuruga amani'' baya na la kuuchokoza na kutojali Umoja wa Mataifa.

Baraza la Usalama linatarajiwa kukutana baadaye leo kujadili jaribio hilo la makombora lililofanywa siku ya Jumapili.

Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kujaribu kombora lake la masafa ya kati, ambalo lilipaa karibu kilomita mia tano kabla ya kutua katika bahari ya Japan.