Park Geun-Hye na tuhuma za rushwa

Park Geun-Hye Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Park Geun-Hye

Rais wa zamani wa Korea kusini Park Geun-Hye amefikishwa kizimbani, kuhusiana na kesi inayomkabili ya tuhuma za rushwa.

Ni muonekano wake wa kwanza hadharani toka alipotolewa madarakani na kukamatwa mwezi wa tatu.

Bibi Park na msiri wake Choi Soon-Sil wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya madaraka na rushwa.

Waendesha mashtaka wanasema waliyashinikiza makampuni kuchangia fedha katika taasisismbalimbali na baadaye kuzitumia kwa faida zao.

Park Geun-Hye anatuhumiwa kwa kuchukua mamilioni ya dola kama hongo ikiwemo kutoka kampuni ya Samsung.

Wote kwa pamoja wamekanusha tuhuma dhidi yao.