Mshukiwa wa shambulio la Manchester atajwa

Manchester explosion Haki miliki ya picha Peter Byrne
Image caption Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza

Mshukiwa wa shambulio la Manchester ametajwa kuwa ,Salman Abedi, ambaye ni mzaliwa wa Manchester mwenye umri wa miaka 22.

Ana ndugu mkubwa aliyezaliwa mjini Landon na wadogo zake waliozaliwa Mjini ,Manchester.

Familia yake inadaiwa kuwa na mizizi nchini Libya.

Wameishi katika maeneo tofauti mjini Manchester ikiwemo jumba lililopo barabara ya Elsmore katika eneo la Fallowfield ambalo lilivamiwa na polisi siku ya Jumanne.

Majirani wamesema vile familia hiyo imekuwa ikipeperusha bendera za Libya katika nyakati tofauti za mwaka.

Polisi katika mji wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 22 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kwenye mulipuko huo ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.

Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.

Haki miliki ya picha Peter Byrne
Image caption Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza

Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake, wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima.

Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.

Haki miliki ya picha Peter Byrne
Image caption Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza

Eneo kulikotokea mulipuko huo limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza

Ripoti ambazo hazijathitishwa kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao hawakutajawa zinasema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Haki miliki ya picha Peter Byrne

Ukumbi wa Manchester ambao ulikuwa ukifahamika awali kama ukumbi wa wanaume, ndio ukumbua mkubwa zaidi mjini humo wenye uwezo wa kuwachukua watu 18,000

Barabara ya ukumbi huo unuangana na kituoacha treni cha Victoria kati kati mwa mji.

Haki miliki ya picha Peter Byrne
Image caption Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza

Ukumbi huo hutumiwa kuandaa tamasha za manyota wakuu kama Ariana Grande nyota wa runinga mwenye umri wa miaka 23 ambaye sasa ni nyota wa muziki wa pop.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Haki miliki ya picha PAUL ELLIS
Image caption Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza